Habari za Punde

Balozi Seif aandaa dhifa kuwapongeza watendaji wa Wizara yake

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi wa mwanzo kulia Mh. Saleh Nassor Juma akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakijipatia mlo kwenye dhifa maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini.
Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti OMPR – ZNZ Nd. Khatib  Said Khatib, Msaidizi wa Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Iddi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Mh. Subeti Khamis wakiwa miongoni mwa watu walioshiriki dhifa hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wa Ofisi hiyo baada ya kumaliza dhifa maalum waliyoandaliwa watendaji hao.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapongeza watendaji wa Ofisi yake kwa kazi kubwa waliyoifanya kumaliza salama bila ya vikwazo bajeti ya Wizara yao.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi maalum ya Shilingi  Laki 500.000/-Kiongozi wa Kikundi cha Taarab asilia cha Akheri Zamani Msanii Matona Issa Matona baada ya kutumbuiza kwenye dhifa maalum ya Ofisi hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif Mazizini.

Balozi Seif akiagana na baadhi ya wasanii wa Kikundi cha taarab asilia cha Akheri Zamani baada ya kumaliza kazi yao ya burdani kwenye dhifa ya watendaji wa Ofisi yake.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ

2 comments:

  1. Hakiiiiiiii,sawa! hii c haki.Jee wakulima na walala hoi wao jee watafanyiwa dhifa na nani. Dhifa kama hizi ni dhuluma kubwa kwa walala hoi walipa kodi ya visiwa hivi. Mwasema uchumi mbaya lakini fedha za kuziteketeza mnazo.Mwadhani mungu yupo pamoja nanyi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu hapo juu, kwa kweli hata mimi nimepatwa na masuali mengi bila ya majibu. Suali la kwanza nani anadhamini hizi dhifa, je ni kutoka kwenye fedha zao mifukoni yaani ni fedha za Maalim seif na Balozi Sefu Ali Idi au ni kutoka kwenye hazina ya Wazanzibar walio masikini na mafukara wa kutupwa. Ikiwa ni fedha zao mfukoni (angalau afadhali) ila ikiwa ni fedha za walalahoi wakizanzibari hii ni dhulma sana. Hivi tujiulize kuna lipi kubwa la kupongezana, kwani kufanyakazi kwa ufanisi na kupelekea kupitishwa kwa bajeti si ndio wajibu wa wafanyakazi au vipi?? Au tulitarajia tufanye nini humu makazini??

      Halafu suali jengine , hivi lini ilitokea bajeti yoyote ya Wizara ya SMZ kutopita. Mimi kiumri si mkubwa , hebu wakubwa wenye kujua mambo watueleze bajeti ya Wizara ipi ilishibwa kupitishwa na mwaka gani??
      Huu ni ufujaji wa mali ya wanyonge, kila kukicha tunakamuliwa kwa kodi mbali mbali , halafu leo wakubwa wanaziafuna rasilimali za wanyonge kwa urahisi eti kupongezana, kwa kweli hii ni janja tu ya kutaka kuziafuna pesa.
      Pia naanza kupata mashaka na Uongozi wa Maalim, sijui naye anafuata mkumbo tuu?? au vipi napata mashaka kama atakufanikiwa kuiongoza nchi, sijui kama kutakua na mabadiliko ya kweli. kwa dalili kama hizi. Kumbuka alipoulizwa kuhusu ubadhirifu kwenye ofisi yake mwaka jana nadhani majibu yake hayakuwa ya "ki-resposbility" anakumbuka alisema kila mmoja ana idara yake yakufanya kazi yeye huambiwa tuu ndege ile pale na analofanya ni kupanda na kwenda safari tuu. Kwa kiongozi yoyote yule hata sio lazima awe Makamu wa Rais basi majibu kama haya yana mushkel. Hivi kweli kwa utamaduni wetu wa kufanya kazi hapa kwetu na zaidi Africa unasema huna habari ya nini kinafanyika kuhusu matumizi ya Ofisi yako?? Waswahili wataiba mpaka mafaili ofisini. Nasema haya kwa ushahidi kwani nasi tumo humo humo serikalini.
      Uongozi hasa kwenye matumizi ya rasilimali unataka uangalizi na udhibiti mkubwa sana. Fedha nyingi za Umma maofisini hutafunwa kwa vijisababu vya ovyo ovyo tuu, huku mambo muhimu ya utekelezaji wa majikumu muhimu ya kuzalisha mali na kuleta maendeleo katika huduma yakiachwa na kupuuzwa kabisa, huku wakubwa wakijitafunia maposho ya ajabu ajabu.
      Kwa kweli tuna shida sana ya udhibiti wa fedha na raslimali nyengine za umma katika taasisi nyingi hapa Zanzibar, watu hufanya watakavyo. Ukijaribu kuwa mkali nao, tayari kushakuwa mbaya.
      Sijui kama kweli tutafika. Wito wangu kwa wale walio karibu na Maalim, wamzindue, kuna wajanja wengi, wanaweza wakambaribia yeye binafsi lakini kubwa zaidi kuuharibu umma amabo tayari umetopea kwenye umasikini na ufukara uliokithiri.

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.