Na
Shemsia Khamis, Pemba
KESI
za migogoro ya ardhi 771 zimeripotiwa katika mahakama ya ardhi mkoa wa kusini Pemba kuanzia mwaka 2006 hadi 2013.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Ofisa Mdhamini wizara ya ardhi kisiwani Pemba,
Hemed Salum Hemed, alisema kati ya kesi hizo,kesi 555 tayari zimetolewa uamuzi.
Alisema
kesi 261 ndio ziliozsalia katika mahakama hiyo, zikiwa katika hatua mbali
mbali, ikiwemo kusikilizwa na kuitwa mashahidi.
Alisematokea
kuanzishwa kwa mahakama hiyo, inaonekana migogoro inaongezeka siku hadi siku,
kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo ardhi kupanda bei.
Kwa
upande wake, Hakimu wa mahakama hiyo, Salum Hassan Bakar, alisema kuna changamoto
kadhaa zinazowakabili katika kusikiliza kesi
za migogoro ya ardhi, ikiwa ni pamoja na mrundikano wa kesi katika mahakama hiyo.
Akizungumzia
athari zinazojitokeza kutokana na kuwepo kwa mogogoro ya ardhi katika jamii,
alisema ni pamoja na kuongezeka chuki na hasama kwa wana jamii.
Nae Karani wa mahakama hiyo, Seif Kassim Said,
akitoa takwimu za kesi zilizoripotiwa mahakamani hapo, kuanzia mwaka 2011 hadi
mwaka 2013 alisema jumla ya kesi 263 ziliripotiwa.
Alisema
mwaka 2011 ziliripotiwa kesi 107, wakati mwaka 2012 ziliripotiwa kesi 61 na mwaka 2013
ziliripotiwa kesi 95.
No comments:
Post a Comment