Na Kadama Malunde,Kahama
MWANAMKE mmoja mzee mkazi wa
Nyahanga,wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Rebeka Shija (82), ameuawa kikatili kwa kukatwa kwa shoka
kichwani na mke wa mtoto wake, aliyejulikana kwa jina la Magreth Richard (30).
Walioshuhudia tukio walisema limetokea jana majira ya saa 3:00
asubuhi katika mtaa wa Nyahanga, mjini Kahama ambapo marehemu Rebeka Shija
alienda nyumbani kwa mtoto wake wa kiume, Bundala Sengasenga (46) alikokuwa
ameitwa na mkwewe kumsaidia kuanika dengu.
Mashuhuda hao walisema marehemu alikuwa
akiishi kwa mwanawe mkubwa, Stanley Sengasenga,katika mtaa huo.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo, alisema mama
mkwe wake alifikia sebuleni na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye
hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia na alipoangalia alimkuta mkwewe akiwa ameuawa.
Imeleelezwa kuwa kabla ya tukio, mtuhumiwa
ambae kwa sasa anashikiliwa na jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga kwa mahojiano, alikwenda
nyumba ya jirani yake aitwaye Noeli Mkisi kuazima shoka kwa ajili ya kuchanja
kuni.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza
shoka hilo
baadaye lilikutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.
Imeelezwa kuwa shoka hilo lilipatikana baada ya mbinu za
kiupelelezi za jeshi la polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo
baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika
mwelekeo ambao mtuhumiwa alielekeza.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,
Kamishina Msaidizi wa Polisi, Kihenya Kihenya alisema marehemu aliuawa kwa
kukatwa shoka kichwani na mtuhumiwa ambaye ni mke wa mtoto wake.
Alisema baada ya mauji hayo mtuhumiwa
alimuacha marehemu sebuleni kisha kutumbikiza shoka alilotumia kufanya unyama
kwenye tenki la kuhifadhi maji.
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni imani
za kishirikina.
Wakati huo huo mwanamme mmoja
asiyejulikana jina wala makazi yake (25-30) amekutwa ameuawa kwa kushambuliwa
kwa mawe.
Aise watanganyika ni makatili. Yaani we acha tu. Hizi balaa zao wasituletee Zanzibar.
ReplyDelete