Habari za Punde

    MAKUTANO YA FIKRA JUU YA RASIMU YA KATIBA

Kama mjuavyo, mchakato wa kupata katiba mpya umekwama katika Bunge Maalum la Katiba kutokana na kushindwa kupatikana kwa theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono pendekezo la CCM kuhusu Rasimu ya Katiba. Kama hili halitoshi, ususiaji wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka kundi la UKAWA, umezidi kuathiri vibaya mchakato mzima wa kupata katiba mpya ya nchi.

Kwa madhumuni ya kutafuta njia zitakazosaidia kufanikisha jitihada za kupata katiba mpya, napenda kukujuilisheni kuwa ZIRPP, kwa ufadhili wa “The Foundation For Civil Society”, imeandaa mkutano wenye maudhui yaliyotajwa hapo juu na inakualikeni kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika mjadala utakaojitokeza katika mkutano huo ambao utafanyika siku ya Jumapili tarehe 06 Julai 2014 katika Ukumbi wa Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, hapo Vuga, Zanzibar, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana.

Ratiba ya mkutano pamoja na nyaraka nyingine zitatolewa siku ya mkutano.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo muhimu atakuwa Mheshimiwa Hassan Nassor Moyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano.

Natanguliza shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wako.


      (Muhammad Yussuf)
MKURUGENZI MTENDAJINo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.