Habari za Punde

Madereva kuzingatia Sheria za Barabara

 Wanafunzi wa skuli ya kiembesamaki wakivuka barabara katika eneo la alama maalum ya barabara kuruhusu watembea kwa miguu kuvukia eneo hilo.
 Kuna baadhi ya madereva hukiuka alama za barabara wakati wakiwa katika matumizi ya barabara hizo hasa katika alama za zebra cross hawafuati alama hizo kama inavyoonekana katika barabara ya kiesmbesamaki wanafuzi wakivuka barabara hiyo na baadhi ya hupita na kupuuza watembea kwa miguu wakati wakitumia alama hizo.

2 comments:

  1. hapo hamna lolote, kama kweli serekali inataka sheria zifatwe basi waweke adhabu kali kupita kiasi, tuone kama sheria hazitofuatwa lakini leo mtu anavunja sheria kwa kuwa yeye ni mtoto wa fulani au atatoa rushwa kidogo tu, basi hata mimi sitofata sheria, angalia mfano uk ukifanya kosa unajua kuna kiasi fulani ukilipe ukikichelewesha kinazidi, mbona kila mtu huweka akili yake vizuri, serekali ndio ya kulaumiwa hapo, jengine watu wanapuuza sheria za barabarani kwa kuwa hawazijui kwa sababu mtoto wa fulani anapasishwa wakati yupo nyumbani au skuli pengine hata umri wa kutumia hivyo vyombo hajafika tunawaona watoto wadogo wanaendesha magari, miaka 13, 15 unafikiria ata ana akili ya kufikiria hatari?, uk mke wa waziri mkuu keshapigwa penalty kwenye train just kapoteza tikket yake tu, na sheria inasema anipo kuja muangalizi wa ticket lazima umuonyeshe sasa kama huioni au hujui umeiweka wapi inakuwa kazikwako, sheria haina mkubwa kila mtu awe chini ya sheria ndio tutakwenda.

    ReplyDelete
  2. kama huyo bwamkubwa keshaona watoto wanataka kukata njia lakini hajui kupunguza wala kusimama, atakuja na moto wake tu hafikirii labda mtoto anaweza asimuone akakata njia ghafla, sababu anajua hakuna atakachofanywa, inakuwa tabu kwa sisi tunokaa nje na watoto wetu tushazoweya sheria huku kama kijisheria cha zebra crossing watakuja kukata njia wauliwe bure, hakuna mtu anaechukuwa tahadhari ya jambo lolote watu wangapi washauliwa na madereva wazembe ikisha kikubwa wanasema sorry,bahati mbaya, Mungu ndio alopanga, nk ujinga mtupu hamna bahati mbaya yoyote ni uzembe tu kama si wa dereva basi wa mpasishaji au serikali, inasikitisha sana.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.