Habari za Punde

Chuo cha Biashara Dae-es-Salaam (CBE) Chatoa Msaada kwa Wadi za Wazazi na Watoto Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ikiwa ni Kuadhimisha miaka 50.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Kuu ya Mnazmmoja Dkt. Jamala Adam Taib akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Biashara cha Dar es Salaam Prof. Emanuel Amani Mjema wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashuka  ya wodi ya akinamama na watoto ikiwa ni maadhimimisho ya miaka 50 tokea kuanzishwa chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Biashara cha Dar es Salaam Prof. Emanuel Amani Mjema akitoa maelezo kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo  katika hafla ya kukabidhi mashuka katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Zanzibar, kulia ni  Naibu  Mkuu wa Chuo hicho anaeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Dkt. Esther R. Mbise
Mkuu wa Chuo cha CBE  Prof. Emanuel Amani Mjema akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi msaada wa mashuka uliotolewa na chuo hicho kwa ajili ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Chuo cha CBE  na baadhi ya maafisa wa Hospitali  ya Mnazimmoja .


Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis akiagana na Mkuu wa Chuo cha CBE baada ya kukabidhiwa mashuka kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto  Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.