Na Waandishi wetu, ZJMMC.
“Hivi
unaweza kuamini kuna watu wanatoka Dar-es-salaam na kuja Zanzibar kwa ajili ya
kufuata pembea?”
Ndugu Mussa Yussuf Mussa afisa habari mkuu wa mfuko wa
hifadhi ya jamii Zanzibar, aliyasema hayo yalipofanyika mahojiano maalum katika
ofisi za ZSSF(ZANZIBAR SOCIAL SECURITY FUND) makao makuu Kilimani, Manara wa
Mbao Zanzibar.
Alianza mazungumzo yetu kwa kusema kuwa mnamo tarehe 3
Septemba, 2008. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais wa wakati huo
Mh.Dk.Amani Abeid Karume, aliamuru viwanja vya Uhuru Kariakoo Amusement Park
viwe chini ya usimamizi wa ZSSF. Baada ya baadhi ya wafanyabiashara kuomba
vibinafsishwe kwao ili waviendeshe.
Alisema mwaka 2008 ZSSF walianza ukarabati mdogo wa
viwanja hivyo vya kufurahisha watoto. Na vikaanza kazi kwa muda kukiwa na
pembea tano. Kama Chairtour, Pembea ya farasi, Pembea ya vikapu na nyinginezo.
Alisema ZSSF wamepewa jukumu hili la kukiendesha
kiwanja hicho likitoka katika usimamizi
wa Wizara ya Habari Utalii utamaduni na michezo tangu mwaka 1980 hadi
ilipokabidhiwa rasmi kwa ZSSF mwaka 2008.
Alisema Historia ya viwanja hivi inatokana na sera za
chama cha Afro-Shirazi (ASP) katika harakati zake za kustawisha hali za
wananchi zifanane na pia kuwaangalia watoto wa wafanyakazi na wakulima.
“Iwapo ASP itakapopata
madaraka ya serikali itazingatia ustawi wa jamii katika hali iliyobora.”
Afisa habari mkuu wa ZSSF bwana Mussa Yussuf Mussa alinukuu hali ilivyokuwa
hapo zamani.
Alifahamisha kuwa baada ya kupata madaraka serikali ya
chama cha ASP mwanzoni mwa miaka ya 1970 waliweza kutekeleza mambo mbalimbali
katika kustawisha hali za wananchi kama kujengwa kwa majengo ya Michenzani
yanayotumika kwa makazi hadi hii leo.Kusimamia ununuzi wa meli ya M.V
Maendeleo, Mapinduzi na Ukombozi.
Ujenzi wa viwanja vya uhuru maarufu kwa jina la
Kariakoo ulipewa jina hilo baada ya
kuwepo katika eneo la Kariakoo mjini Zanzibar.
Alieleza kuwa ujenzi ulianza mwaka 1974 ukakamalika mwaka 1975 katika
kipindi cha serikali iliyokuwa inaongozwa na Rais wa wakati huo Mh .Aboud Jumbe
Mwinyi ikisimamiwa chini ya halmashauri
ya uingizaji zana za ujenzi.
“1976 kiwanja cha Kariakoo kilianza rasmi kazi ya
kufurahisha watoto na watu wazima kukiwa na pembea saba,” alifahamisha.
Hata hivyo, Afisa huyo wa uhusiano wa ZSSF alieleza
kuwa Kuna kipindi kiwanja kilipoteza umaarufu na kuchakaa, kutokana na
usimamizi mbaya wa wakati huo; na hata suala la kugharamia uendeshaji wa
kiwanja hicho ilishindikana.
“Enzi zile wananchi hawakuwa na jukumu la kulipia
wanapoingia ndani ya kiwanja. Lakini sasa kutakuwa na gharama za kuingilia pia
kutumia pembea. Hii itasaidia katika kumudu mahitaji ya uendeshaji pia
kulipatia taifa pato lake ili kuleta maendeleo na ustawi uliobora kwa jamii,”
alisema Mussa akionesha kuwepo usimamizi imara wa kukusanya mapato.
Alisema matumaini yameanza kurudi baada ya miaka mitatu ya kufungwa kiwanja
hicho kwa ajili ya ujenzi mpya na Sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia tisini.
Alisema ZSSF imefanikiwa kutekeleza moja ya majukumu
yake ya kuwekeza fedha zinazotokana na michango kwenye miradi yenye faida kama
itakavyo idhinishwa na bodi ya wadhamini wa ZSSF.
Alisema katika mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho cha
watoto; Bilioni 13 zinakadiriwa zitatumika kukamilisha mradi huo, unaotarajiwa
kukamilika mwezi January au februari
2015.
Alisema kampuni ya CRJE kutoka china iliingia mkataba
na ZSSF 24 oktoba 2012 wa kandarasi ya ujenzi wa miundombinu. Pia kampuni
nyingine ya GOLDEN HORSE imeingia mkataba kwa ajili ya kufunga mapembea.
“utakapo kamilika uwanja huo kutakuwemo na michezo
mbalimbali kama video games, water slides na mapembea ya aina mbalimbali,” aliyasema
hayo ndugu Abdallah Juma afisa habari ZSSF makao makuu.
“kuna kadiriwa kutakuwepo na pembea zipatazo 16. Kama
vile
Airbike, Gerry fish, Sky diver, Viking, Pambercar,Supersewingna
nyinginenyingi,” aliongezea katika ufafanuzi wake ndugu Abdallah Juma.
Aidha alisema tarehe 26 Septemba,2014 haitosahaulika;
kwani majaribio ya kutumika kiwanja kipya cha NEW ZSSF UHURU KARIAKOO AMUSEMENT
PARK yalifanyika kwa muda wa siku 5. Na pembea zipatazo 12 zilitumika katika
uzinduzi huo.
Mussa alisema
ili kuhakikisha msaada wa haraka unaweza kupatikana endapo kama kutatokea
tatizo lolote, ZSSF walifuata ushauri uliotolewa na rais wa serikali ya
mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed.Shein
kuzipatia ufumbuzi nyumba zote zilizogandamana na uwanja huo kwa kuzinunua.
“Ushauri wa mkubwa ni agizo,” alisema afisa habari
mkuu wa ZSSF makao makuu.
Alieleza kuwa hivi sasa kiwanja kimekuwa na eneo la
kutosha nje. Ndani hakuna majengo yaliyo kama tube ili kuepuka matatizo
mbalimbali ya kimazingira kama magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya hewa.
Akielezea mambo mengine alisema kutakuwemo na maduka
yatakayouza vitu vya watoto kama toys,mkahawa wa chakula na ukumbi utakao
tumika kwa mikutano, harusi, na shughuli mbalimbali.
“Tukumbuke hii ni sehemu ya kufurahisha watoto mambo
yanayofaa katika eneo hili ni yale yatakayo endeleza furaha ya watoto. Hivyo
haifai kuuzwa kwa vileo ama kuvitumia vitu kama sigara, bangi, viroba n.k.
kwani matumizi ya mihadarati kwa uwazi mbele ya watoto itaharibu malezi na
maadili yao”. alisema
Juu ya ajira alisema “Ajira tumezigawa sehemu kuu
mbili skilled na unskilled. Hivi mfagiaji anahitaji elimu, pia kutakuwepo na
ajira nyingine zitakazotokana na maduka tutakayo kodisha,” alifahamisha afisa
habari mkuu ndugu Mussa Yussuf Mussa.
Alisema inakadiriwa kupatikana ajira maalum za moja
kwa moja 50 ndani ya kiwanja hicho katika maeneo ya utawala, mafundi na wale
watakao ongoza watumiaji wa pembea na michezo mbalimbali.
Kuhusu usalama alisema kuna CCTV kamera zenye uwezo wa
kuchukua, kurekodi matukio mbalimbali ndani na nje ya uwanja; pia jeshi la
polisi na vyombo vingine vya ulinzi vitasaidia kuhakikisha ulinzi unapatikana
ndani ya kiwanja kwa kipindi chote cha michezo.
“Mabomba maalum ya kutolea matangazo yatakuwemo ya
kutosha ili kurahisisha suala la kutoa matangazo mbalimbali pale yatakapo
hitajiaka. Pia kuna milango ya dharura ya kutosha itakayotumika endapo litatokea
jambo si la kawaida,” alifahamisha.
Akielezea huduma za kiafya alisema msalaba mwekundu,
madaktari mahiri watatoa huduma za kiafya ndani ya kiwanja pindi mtu atakapo
pata tatizo la kiafya, iwe kuanguka, kuumia na mengineyo.
“yeyote atakapopata tatizo la kiafya ndani ya kiwanja
tutamshughulikia kwa kutumia wataalamu tuliokuwa nao, endapo tatizo litakuwa
kubwa tutampeleka hospitalini kwa gharama zetu.” Alizungumza kwa msisitizo
afisa habari mkuu wa ZSSF makao makuu.
Hata hivyo,ndug Abdallah Juma alisema idadi ya watu
elfu sita inakadiriwa kuwa wataingia kwa wakati mmoja ndani ya kiwanja hicho
kwa kujumuisha wale watakaokuwa wanatumia pembea na wanaotumia maeneo mengine.
“Kiwanja kinadhaniwa kitaweza kufanya kazi kwa muda wa
siku 7 za wiki. Kitafungwa saa 3 usiku kwa siku za kawaida na saa 4 kwa siku za
sikukuu kitakapoanza rasmi kazi,” alifahamisha namna kitakavyofanya kazi huku
akisema jambo hilo bado halijadiliwa kwa kina hadi pale watakapo kabidhiwa,
ndugu Mussa.
“Njia mbalimbali zitatumika kukitangaza kiwanja hicho
ndani na nje ya Zanzibar kupitia traditional media, social media, blogs na word
mouth”, aliongeza.
Alisema kiwanja hiki kitaongeza thamani ya visiwa vya
Zanzibar katika sekta ya utalii pia kustawisha hali bora za wananchi katika
michezo mbalimbali pia burudani. Alisema kitavutia sio tu kwa wakazi na wenyeji
wa Zanzibar, lakini pia wale wanaotoka ndani na nje ya bara la Afrika.
“Zanzibar tumebarikiwa kuwa na sehemu mbalimbali za
kupumzika na kufurahi kama jamuhuri garden, forodhani na kariakoo kwa unguja”,
alisema
Hata hivyo, alisema si mradi huu wa NEW ZSSF UHURU
KARIAKOO AMUSEMENT PARK pia upo mwingine unaoendelea katika ujenzi kisiwani Pemba
kwenye uwanja wa UMOJA uliopo kwenye eneo la tibirinzi.
“Yatupasa tufahamu na tuzingatie kiwanja hiki kitakapo
kamilika na kukabidhiwa rasmi kwa ZSSF ni mali yetu sote wakazi wa Zanzibar
hatuna budi kukitunza kwa lengo la kutuburudisha , kujifunza, kuendeleza
mahusiano bora kati ya jamii na taasisi za serikali,” alitahadharisha afisa
huyo wa habari mkuu wa ZSSF.
Alisema ujenzi haujakamilika na watu wasiwe na
wasiwasi kwa baadhi ya mapungufu yaliyojitikeza kipindi cha majaribio. na
inshaallah kila kitu kitakamilika kama ilivyopangwa.
“kimejengwa kwa
ajili yao; kitunze kidumu, suala la kukitunza tusiachiwe peke yetu,” alihitimisha
mahojiano yetu kwa kauli hiyo ndugu Mussa Yussuf Mussa afisa habari mkuu ZSSF
makao makuu.
Makala haya ya Imeandaliwa
na HARUNA OMARY SAID mwanafunzi chuo cha habari Zanzibar anapatikana kwa namba
0659 526 004,
Na kuhaririwa na MOHAMMED MZEE mwalimu chuo cha habari Zanzibar.
Shukrani ziwaendee.
1. LUCAS ANDREW MKUI.
2. ATIE ALI KHAMIS.
3. MWAPILI VITUS.
4. ALLY YAHAYA ALI.
5. MARYAM RAJAB BAKAR.
6. UMMUL-KULTHUMU IBRAHIM OTHMAN.
7. HIDAYA KHAMIS MSHENGA.
Kwa kushirikiana nami katika
kutafuta taarifa zote za muhimu za kukamilisha makala haya yaliyonichukua
takribani saa 96 hadi kukamilika kwake huku nikikutana na changamoto nyingi za
kunikatisha tama.
Pia shukrani kwa
1.
MASHA ALI MUSSA(Dada yangu na
msimamizi wa kazi zangu)
2. MWAJABU IDDI(Mama, kunitia moyo usiku
na mchana kipindi nafuatilia mambo mbalimbali)
3. THABIT MADAI(Kwa kunichangia mawazo
kipindi naandika makala haya)
4. ALI MASOUD(Kunisaidia ufundi wa
laptop yangu kipindi chote bila kusita)
5. Wanafunzi wa cheti chuo cha habari
Zanzibar 2014/2015 kwa ushirikiano wao.
6. MAKAME USSI SHOMARI(Mwl. Wa Kiswahili
chuo cha habari Zanzibar )
7. SALEHE R. KOSHUMA(Mshauri wangu
mkubwa, mwl. Chuo cha habari Zanzibar )
8. HANIFA
9. YUSUF SIMAI ISSA(Mdogo wangu).
Nakusii endelea
kumakinika nami katika muendelezo wa makala za mithili yako hapana na hatua
zangu ndani ya mji mkongwe nikiangazia mambo mblimbali ya kijamii, kisiasa,
uchumi na historia, burudani hata tamaduni.
No comments:
Post a Comment