Habari za Punde

Maadhimishi ya Wiki Maji Jimbo la Makunduchi.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ra Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mh. Haroun Ali Suleiman,ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Unguja (CCM),akiangalia ramani ya uchimbaji wa msingi wa kupitishia mabomba ya maji kutoka katika pango la maji la Mnywambiji na kuelekea kwenye vijiji vya Makunduchi na Kibuteni ,ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Maji Duniani
MJUMBE wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Makunduchi Unguja Mh. Haroun Ali Suleiman,akikata kitawi cha mti kuashiria uzinduzi wa uchimbaji wa msingi unaotoka kwenye pango la Mnywambiji Kibuteni na kusambaza maji katika vijiji vya Makunduchi na Kibuteni katika Jimbo la Makunduchi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma,ambae pia ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Mh. Haroun Ali Suleiman,akishiriki kwenye uhamasishaji wa uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ulazaji wa bomba la maji katika vijiji vya Makunduchi na Kibuteni huko katika pango la Mnywambiji,ikiwa ni siku ya kwanza ya wiki ya Maji Duniani

KIJANA Jecha Haji Hassan mkaazi wa Makunduchi akichimba msingi huo eneo la miamba huko Kibuteni. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.