Habari za Punde

Waganga wa tiba asili watakiwa kushirikiana na madaktari wa Afya

 Mwenyekiti wa Shirika la World Doctors kutoka Italia Bi. Tanya Niestedt (kulia) akizungumza na Waganga wa Tiba asili hawapo pichani katika semina ya siku moja ya yakuwataka waganga hao washirikiane na Madaktari katika kutibu magonjwa ya Kisukari na Presha, kushoto ni Mkuu wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza Zanzibar Dkt. Omar Mwalim, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
 Mkuu wa kliniki ya Kisukari Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Faiza Kassim (aliesimama) akizungumza na Waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuhusu mashirikiano ya utibabu wa magonjwa ya kisukari na presha.Ili kuepuka mgonjwa mmja kutumia dawa za Hospitali na zile zinazotolewa na waganga hao. 

Mmoja wa Waganga wa Tiba asili Bi. Zahra Hassan Ali akichangia katika semina hiyo iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


1 comment:

  1. Huyo mkuu wa maradhi yasiyoambukiza sio dokta jamani.zanzibar mtu yeyote afanyae kazi hospitali wakati mwengine hata wizara ya afya,ataitwa dokta.tubadilike

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.