Habari za Punde

Mkutano Mkuu wa Wadau wa Mfuko wa Jamii wa Zanzibar ZSSF Bwawani Zanzibar,

                                                                                                   
                                                                                              

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Ndg Mussa Yussuf, akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa ZSSF uliofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani kwa Uzinduzi wa Mafaoo ya Uzazi na Uchangiaji wa Hiari kujiwekea hakiba ya Uzeeni Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungua Mafao ya Uzazi na Uchangiaji wa Hiari katika Mfuko wa ZSSF, uzinduzi huo umefanyika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Dk. Mwinyihaji Makame, Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF,Dk. Suleiman Rashid Mohammed na Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Ndg, Mwadini Makame, wakishangilia baada ya kuzinduliwa Mfuko wa Uzazi na Uchangiaji wa Hiari. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Dk. Mwinyihaji Makame, Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF,Dk. Suleiman Rashid Mohammed na Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF Ndg, Mwadini Makame, wakisoma bango lenye ujumbe wa Wajasiriamali mbalimbali wakiwa katika shughuli zao za uzalishaji. ambao ni Wachangiaji wa Hiari Mfuko wa ZSSF.kwa kujiwekea hakiba ya uzeeni. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Dk. Suleiman Rashid Mohammed, akikpokea mfano wa Cheki ya shilingi miliono tano kwa ajili ya kuchangia Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadauu wa ZSSF,kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi,na katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Ndg Mwadini Makame na kulia  Afisa Mawasiliano wa Benki ya Posta Bi Noves. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa mkutano huo kuelezea huduma zao wanazotowa kwa Wadau wao Wanachama wa ZSSF Zanzibar kwa kutowa mikopo kupitia Benki ya Posta na kurahisisha malipo ya mafao kwa Wanachama wa ZSSF.

























No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.