Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimskiliza mgeni rasmi katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika uwanja wa mpira wa Dimani leo,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika uwanja wa mpira wa Dimani leo,[Picha na Ikulu.]

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akiwaombea kura Viongozi wa CCM walioomba nafasi za Uongozi katika kamapeni za CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa mpira Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Jimbo la Dimani,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shei,[Picha na Ikulu.]
Maelfu ya Wananchama wa CCM na Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao leo,[Picha na Ikulu.]

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt.Mohamed Seif Khatib alipokuwa akiwasalimia wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Dimani katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika le katika uwanja wa mpira Dimani Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.]
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akiwaombea kura Viongozi wa CCM walioomba nafasi za Uongozi katika kamapeni za CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa mpira Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Jimbo la Dimani,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shei,[Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 19.10.2015

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamewaeleza wanaCCM na Wananchi kuwa
hakuna chama chenye historia,kujali maslahi na maendeleo ya wananchi isipokuwa
CCM hivyo kuna kila sababu ya wao kuwachagua viongozi wa chama hicho wanaogombania
nafasi za uongozi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika
mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na
wanaCCM uliofanyika uwanja wa Mpira Dimani, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini
Magharibi ambapo mgeni rasmin alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM Dk. Ali Mohamed Shein.
Nae Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohammed
Seif Khatib alisema kuwa hakuna chama hata kimoja chenye historia ya ukombozi
isipokuwa chama cha CCM ambacho kinawajali na kinawathamini wananchi.
Alisema kuwa CCM ina Sera thabiti kwani
inayatambua na inayathamini Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambapo pia, chama
hicho kimezaa Muungano ambao umeleta umoja na mshikamano hadi hivi leo.
Alisema kuwa CCM ina kila sababu ya
kuingia Ikulu kwani mgombea wake wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk.
Ali Mohamed Shein ana kila sifa, elimu ya juu ya Sayansi, ana Digirii tatu, mtu
wa watu, mpole na myenyekevu na anawapenda Wazanzibari, si mbaguzi.
Nae Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Idd alisema kuwa uhuru wa Zanzibar umepatikana kutokana na wakulima na wakwezi
hivyo hashangazwi na viongozi wa chama cha CUF kumwambia kuwa andapo watapa
nchi akatafute jembe akalime.
Balozi Seif pia, alishangazwa na chama
cha CUF kusema kuwa Zanzibar hakuna maendeleo na kueleza kuwa maendeleo yaliopo
hivi sasa hawayaoni.
Balozi Seif alisema kuwa tayari kuna
baadhi ya wafuasi wa chama cha CUF wameshadhamiria kufanya fujo na hivi sasa
tayari wameshawahamisha watoto wao kuwapelekea Pemba ili wao wabakie kwa lengo
la kufanya vurugu.
Alisema kuwa Chama cha CUF kimejiandaa
kuwadhibiti wafuasi wa CCM siku ya uchaguzi na kueleza kuwa CCM imeshapata habari
na vyombo vinavyohusika katika kusimamia amani na utulivu vitawashughulikia
wale wote watakao leta vurugu.
Aidha, Balozi Seif alitumia fursa hiyo
kuwaombea kura wagombea wote wa CCM.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai
Ali Vuai alitoa pongezi kwa wanaCCM kwa kushiriki vyema katika mikutano ya
chama hicho na kueleza kuwa kuna kila sababu ya ushindi wa CCM.
Nae Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Magharibi,
Yussuf Mohammed, alisema kuwa CCM itashinda kwa ushindi mkubwa katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
Alisema kuwa uwanja wa mpira wa Bweleo
umetengezwa na Serikali ya CCM na kushangazwa
na ahadi zilizotolewa na viongozi wa CUF kujenga uwanja huo ambapo ahadi
hizo zote zilikuwa hewa na badala yake Serikali chini ya CCM umekijenga kiwanja
hicho.
Alisema kuwa Mapadri, Maaskofu na
Wachunganyi amani yao iko kwa CCM na sio chama cha CUF kwani chama hicho hawana
imani nzuri na watu wa dini ya Kikiristo kutokana na maovu mbali mbali
waliowafanyia watu wa dini hiyo hapa nchini.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment