Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini na kutafuta wakulima bora wa zao la Karafuu ambae pia ni Mkurugenzi Idara ya Kilimo Zaki Khamis Juma akitoa maelezo juu ya mchakato uliotumika katika kuwapata wauzaji na wakulima bora wa zao la karafuu.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Baadhi ya Wakulima na Wauzaji bora wa zao la Karafuu wakimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Bi. Mwanahija Almas Ali (hayupo pichani) wakati wa kukabidhiwa zawadi wakulima bora wa zao hilo kwenye sherehe iliyofanyika katika Ofisi zao ziliopo eneo la kwa Abass Hussein Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Bi Mwanahija Almas Ali akimkabidhi zawadi Mkulima bora wa zao la Karafuu Iddi Mohd Issa kutoka Wilaya ya Magharibi Unguja kwenye hafla iliyofanyika Ofisi za ZSTC kwa Abass Hussein Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wakulima na Wauzaji bora wa zao la Karafuu wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa na Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar kwa kushirikikiana na Idara ya Kilimo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment