Habari za Punde

Kilele cha Matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM Kuadhimisha Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar Viwanja vya Maisara Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akiwasili katika viwanja vya Maisara kupokea Matembezi ya Vijana, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania Sadifa J Khamis , kushoto na kulia Makamu Mwenyekiti wa Chipukizi Tanzania Pili Hassan Suluhu na Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika Jukwaa wakati ukipigwa wimbo wa Taifa.
Vijana wa Chipukizi Zanzibar wakitowa heshima wakati wa kupingwa wimbo wa Taifa wakati wa mapokezi ya Matembezi ya Vijana katika viwanja vya Maisara Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikaguwa Vikosi vya Chipukizi wakati wa Kilele cha Matembezi ya Vijana katika viwanja vya Maisara Zanzibar. 
Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakipita mbele ya mgeni Rasmin Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati akipokea Matembezi hayo katika viwanja vya Maisara Suleiman Zanzibar. wakiwa na Picha za Viongozi. 
Vijana wakiwa katika Matembezi wakipita mbele ya mgeni rasmnin. 
Vijana wakiwa katika matembezi hayo wakiingia katika viwanja vya Maisara kukamilisha matembezi hayo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wakiwa katika matembezi hayo wakiingia katika viwanja vya Maisara kukamilisha matembezi hayo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wa Umoja wa Vijana wakimaliza Matembezi hayo kwa kupiga pushapu wakati wa kupokelewa Matembezi hayo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Shein katika viwanja vya Maisara Zanzibar. 
Vijana wakiwa katika matembezi hayo wakiingia katika viwanja vya Maisara kukamilisha matembezi hayo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa picha ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume na Kiongozi wa Matembezi hayo Daud Ismail katika viwanja vya maisara yalipomalizia matembezi hayo ya Vijana, kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi picha ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe Sadiga Juma Khamisi.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akipokea Picha ya Muasisi wa Muungano wa Tanzania Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere, kutoka kwa kijina  wa Matembezi hayo Khadija Nassor.  

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akipokea picha ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Kijana wa Matembezi hayo Abdalla Ali Chum.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa picha ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, kutoka kwa Kijana Rashid Zungo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akipokea bwaride la Vijana wa Chipukizi wakati wa maadhimisho ya Matembezi ya Vijana wa CCM, baada ya kutembelea Mikoa yote ya Kichama Zanzibar  kwa Kuwashirikisha Vijana kutoka Unguja Pemba na Tanzania Bara., yaliomalizikia katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Kikosi cha Bendra cha Chipukizi kikitoa heshima wakati wa bwaride hilo maalum la kupokea matembezi hayo katika viwanja vya maisara Zanzibar.
Vijana wa Chipukizi wakitoa heshima wakati wa matembezi hayo. 
Vijana wa Chipukizi wakipita kwa ukakamavu 

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Vijana wa Chipukizi wakati wa bwaride maalum liloloandaliwa kwa ajili ya kupokea matembezi hayo ya Vijana wa CCM kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kijana wa Chipukizi akipita kwa ukakamavu akitowa heshima wakati wa bwaride hilo.
Vijana wa Chipukizi wa Kikosi cha Ukombozi wakipita mbele ya Mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya Matembezi hayo katika viwanja vya Maisara Zanzibar.
Vijana wa Chipukizi wa Kikosi cha Ukombozi wakipita mbele ya Mgeni wa heshima wakati wa maadhimisho ya Matembezi hayo katika viwanja vya Maisara Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.