Habari za Punde

Makamo wa Rais Mhe Samia akamilisha ziara yake mkoani Geita

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua chanzo na mtambo wa kuchujia maji unaofadhiliwa na kampuni ya Uchimbaji ya Geita Gold Mining (GGM) Mkoani Geita. Kulia Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalangalala Mkoani Geita baada ya kuzindua na kupokea Magreda  yatakayoanza ujenzi wa Barabara ya Geseko itakayoharimu jumla ya Tshs 1.2 Bl hadi kukamilika. Wa pili kulia Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea na kukagua chanzo na mtambo wa kuchujia maji unaofadhiliwa na kampuni ya Uchimbaji ya Geita Gold Mining (GGM)  kabla ya kuzindua mtambo huo katika kijiji cha Nyankanga Mkoani Geita.  kushoto Mkurugenzi Mkuu wa GGM Terry Melpeter, kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita King Msukuma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining Terry Melpeter  kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Geita baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi Mkoani humo leo.  (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.