Habari za Punde

Dk Shein, Ajumuika na Wananchi Katika Maziko ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Ndugu na Jamaa alipofika nyumbani kwa Marehemu kutowa mkono wa Pole na kuwafariji Wafiwa nyumbani kwao Fuoni Michezani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akijumuika na Ndigu na Jamaa wa Marehemu Ramadhani Nyonje Panda Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wakati wa maziko yake.Marehemu Ramadhani Nyonje amefariki wiki iliopita akirudi matibabuni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Ndugu wa Marehemu wakiitikia dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sh, Khamis Haji Khamis akisoma dua kuuombea mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu nyumbani kwake Fuoni Michezani Zanzibar.
Ndungu na Jamaa wa marehemu wakiitikia dua 
Wanafamilia na Ndugu wakiitikia dua. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariki kizukwa alipofika kumpa pole nyumbani kwake Fuoni Michezani Zanzibar leo asubuhi.


















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.