Habari za Punde

Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakiongozwa na Mratib wao (upande wa mkono wa kulia) Fatma Khamis Hemed,  wakiangalia bidhaa mbali mbali za wajasiriamali wa mkoa wa kaskazini Pemba, ambao walifika eneo la Mchanga mdogo, kushuhudia maadhimisho ya siku ya wanawake, yalioandaliwa na kiutuo hicho
Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria, Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, akiwasilisha mada ya umiliki wa mali kwa wanawake,  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliofanyika shehia ya Mchanga mdogo Jimbo la Kojani wilaya ya Wete, ambapo ilitayarishwa na ZLSC,
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada ya haki za wanawake, kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika shehia ya Mchanga mdogo Jimbo la Kojani wilaya ya Wete, ambapo ilitayarishwa na ZLSC
Mjasiriamali kutoka kikundi cha ufugaji na upandaji mboga mboga ‘’Nia njema’’ cha shehia ya Mchanga mdogo bibi Tadim Issa Maligha, akiomba msaada kupitia vikundi vyao,  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliofanyika Mchanga mdogo Jimbo la Kojani wilaya ya Wete, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.