Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa kuhusu“ Kizazi kinachojifunza: Uwekezaji katika elimu kwa dunia inayobadilika”. hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo imeandaliwa na Makamishna 27 akiwamo Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanyika siku ya jumapili Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Rais mstaafu Kikwete akiwa na Makamishna wenzie kushoto ni aliyekuwa Kamishna wa Umoja wa Ulaya Bw. Jose Manuel Barroso na Rais Mstaafu wa Mexico Bw. Felipe Calderon
Sehemu ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti kuhusu Elimu
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akichangia na kuongoza majadiliano kuhusu kipengele cha ujumuishi katika elimu, ambapo alisema ripoti hiyo imeainisha mikakati na mipango ya kuwafikia makundi ya jamii yanayoishi katika mazingira magumu kama vile wakimbizi, wasichana, watoto wa mitaani, watoto walio katika ajira na watoto wanaobaguliwa.
Kamishna Teopista Birungi Mayanja kutoka Uganda ambaye katika mchango wake alisisitiza sana ushirikishwaji wa walimu katika mchakato mzima wa kuifanyia mageuzi sekta ya elimu ili iweze kuwafikia watoto wote. akasisitiza pia umuhimu wa walimu kuachwa watekeleze majukumu yao ya ualimu pasi ya kuingiliwa au kuongezewa majukumu nje ya majukumu yao ya kufundisha
Mwenyekiti wa Kamisheni na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Elimu, Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza,Bw. Gordon Brown akiwasilisha mbele ya washiriki taarifa fupi ya kilichomo kwenye ripoti ya kamisheni yake ambapo suala kubwa lililositizwa katika ripoti hiyo ni uwekezaji wa raslimali fedha kwenye elimu.
Rais Mstaafu Kikwete akisalimiana na Bibi. Ngozi Okonjo- Iwela Waziri wa zamani wa Fedha wa Nigeria
No comments:
Post a Comment