Na Mwandishi wetu, Pemba
Waumini waliomaliza ibada ya hija nchini wametakiwa kuwa mfano wa matendo mema yanayomridhisha Mwenyezi Mungu mbele ya jamii
Wito huo umetolewa na Al-haj ALI HAJI ALI huko katika Msikiti wa Istiqama Mkanjuni Chake chake alipokuwa akizungumza na Mahujaji katika semina ya siku moja ya kutathmini safari ya Hija ya mwaka huu kupitia jumuiya Al haramain Hajj Group
Alhaj Ali amesema ibada ya hija inamfanya Muumini kujifunza na kuelewa Ukubwa wa Mwenyezi Mungu na kuweza kuishi kwa kumtii Yeye na alivyoviumba katika mbingu na ardhi .
Aidha amewataka Mahujaji hao kuutumia uwezo walionao kuwelimisha wengine kwenda kufanya hija ambayo ni lazima kwa kila mwenye uwezo .
Akisoma risala katibu wa jumuiya hiyo Sheikh Hassan Rashid Mohamed ameeleza kusikitishwa na idadi ndogo ya mahujaji wanaojitokeza kwenda kuhiji.
Amesema bado safari ya hija hairidhishi kwa waislamu wa Zanzibar na kuwataka wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kuiendea safari hiyo muhimu
Nao baadhi ya mahujaji waliokwenda hija kupitia jumuiya ya Al haramai wameipongeza jumuiya hiyo kwa kuboresha huduma zao kwa mahujaji wanaowahudumia.
No comments:
Post a Comment