Habari za Punde

ZSSF Yatowa Tunzo kwa Washindi wa Kutoa Jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)Ndg. Abdulwakali Haji Hafidh, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na shindano la kutafuta jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar na kupatikaka washindi watatu kati ya mia tatu waliojitokeza katika shindani hilo la kutoa jina la bustani hiyo ilioko michezani Zanzibar.


Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo ya kutangazwa washindi wa shindano hilo la kutowa jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abdulwakali Haji Hafidh, akimkabidhi Tunzo na fedha taslim mshindi wa kwanza wa ubunifu wa jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, (Mipinduzi Squar) Ndg.Suleiman Ali, kwa kupata nafasi ya kwanza katika kinyanganyiro hicho iliyowashirikisha washiriki 300. hafla hiyo ya kukabidhi tunzo hiyo imefanyika katika Afisi za Makao Makuu ya ZSSF Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abdulwakali Haji Hafidh, akimkabidhi Tunzo na fedha taslim mshindi wa Pili ubunifu wa jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, (Mapinduzi Squar) Ndg.Khami Shaali Chum,katika kinyanganyiro hicho iliyowashirikisha washiriki 300. hafla hiyo ya kukabidhi tunzo hiyo imefanyika katika Afisi za Makao Makuu ya ZSSF Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Abdulwakali Haji Hafidh, akimkabidhi Tunzo na fedha taslim mshindi wa Tatu ubunifu wa jina la Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, (Mapinduzi Squar) Ndg.Hakim Mgeni.katika kinyanganyiro hicho iliyowashirikisha washiriki 300. hafla hiyo ya kukabidhi tunzo hiyo imefanyika katika Afisi za Makao Makuu ya ZSSF Kilimani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.