Habari za Punde

SSRA Yatoa Msaada wa Chakula na Vifaa vya Usafi katika Kituo cha Kulelea Wazee cha Fungafunga Mkoani Morogoro.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (wa tatu kushoto), akizungumza na wazee wa Kituo cha kulelea wazee cha Fungafunga mkoani Morogoro wakati alipofika kituoni hapo kutoa msaada wa  vitu mbaimbali vyakula, vifaa vya usafi, nguo pamoja na sabuni za kufulia.

Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Bw. Ally Masaninga, wakigawa mifuko yenye vyakula kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Fungafunga Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde (kushoto) akimkabidhi fulana Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulelea wazee cha Fungafunga, Bi. Yolanda Komba wakati SSRA ilipotembelea kituo hicho hivi karibu. 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah KibondeMsika(kushoto) akimkabidhi fulana Afisa Msaidizi Mfawidhi wa Kituo cha kulelea wazee cha Fungafunga Bw Rahid Omary wakati wa ziara ya SSRA katika kituo hicho. 
Baadhi ya wazee wanaolelewa na kituo cha wazee cha Fungafunga, wakiwa wamekusanyika kwenye viwanja vya kituo hicho, kusubiri kugawiwa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), hivi karibuni.  
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah KibondeMsika (katikati), akionyesha baadhi ya vitu vilivyotolewa na SSRA kwa wazee wanaolelewa na kituo cha Fungafunga cha Morogoro.  
Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga, akimkabidhi sabuni kwa mmoja ya wazee wanaolelewa na kituo cha Fungafunga cha Morogoro.  
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (wa nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wanaolelewa na kituo cha Fungafunga cha Morogoro, mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula, vifaa vya usafi na sabuni za kufulia.  
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika, akizungumza na wazee wa kituo cha Fungafunga, mara baada ya kukabidhi msaada wa chakula na vifaa vya usafi katika kituo hicho Mkoani Morogoro hivi karibuni

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.