Habari za Punde

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Yatangaza Matokeo.

BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA) YATANGAZA MATOKEO.
Na: Frank Shija – MAELEZO
22/12/2016
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imepitisha na kutangaza matokeo ya watahiniwa 6,282 waliofanya mtihani kati ya tarehe 1 hadi 4 Novemba, 2016 katika ngazi mbalimbali za masomo.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Pius A. Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza nay a Pili katika ngazi ya ccheti cha utunzaji wa  Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.

Awali taarifa hiyo ilieleza kuwa watahiniwa waliokuwa wamejisajili kwa ajili ya kufanya mitihani ni 6.917 ambapo kati yao watahiniwa 653 sawa na asilimia 9.2 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa watahiniwa 263 kati ya 6,282 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu katika mkao mmoja huku wengine 281 sawa na asilimia 4.4 wakifaulu katika mitihani yao waliyokuwa wameshindwa awali.
Pamoja na ufaulu huo baadhi ya watahiniwa 2,119 wameshindwa katika baadhi ya masomo yao huku 2,898 sawa na asilimia 46.1 wakishindwa kabisa mitihani yao.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imetangaza matokeo haya kufuatia uthibitisho wake ulitolewa katika kikao cha kawaidia cha 170 cha Bodi hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.