Habari za Punde

Mafunzo ya usimamizi wa karakana kwa wakuu na walimu wa vyuo vya amali yafanyika Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

Wakuu na walimu wa vyuo vya amali wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kuwapa uwezo vijana kuweza kujiajiri wenyewe.

Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya vyuo vya amali Zanzibar Dk Bakar Silima ameyasema hayo huko katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya amali Vitongoji  katika mafunzo ya usimamizi wa karakana kwa wakuu na walimu wa vyuo vya amali vya Vitongoji na Dodeani kisiwani Pemba.

Bakar amesema ili kuweza kulifikia lengo hilo baada ya Serikali kuweka miundo mbinu ni lazima kuwepo wataalamu wa kuweza kufundisha kitaalamu na wanaoweza kwenda na wakati.

Naye mkurugenzi wa mafunzo wa mamlaka ya vyuo vya amali Zanzibar Kombo Sheha amewataka walimu hao kuitumia nafasi hiyo ya mafunzo katika kuleta mabadiliko ya kitaaluma katika kazi yao ufundishaji.

Mapema akitowa maelezo katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mdhamini wa Mamlaka ya vyuo vya amali Pemba Othman Zaid Othman amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu hao kuweza kuleta maendeleo ya kitaaluma kwa walimu vijana na Taifa kwa kuwa walimu hao wataweza kujenga uwezo mzuri wa kuziendesha karakana zilizopo vyuoni hapo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.