Habari za Punde

Balozi Seif Awasili Zanzibar Akitokea Ziarani Nchini China

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitoa Nchini China baada ya kumaliza ziara ya siku Tano ya Kiserikali.
Kulia ya Mh. Ayoub ni Meya wa Manispaa ya Mjini Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib na Waziri wa  Kazi Uwezeshaji, Wazee, Vijhana na Watoto Mh. Maudlin Cyrus Castico.
Balozi Seif akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza.
 Balozi Seif akisalimiana na Timu ya Wazee waasisi wa Chama cha Mapinduzi.
Balozi Seif  kulia akiwa makini kusikiliza Maswali mbali mbali aliyoiulizwa na Wana Habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Nchini China.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed aliyembatana naye katika ziara hiyo ya Kiserikali ya siku Tano.
Picha na – OPMR – ZNZ.
Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kukamilika kwa ujenzi wa miradi mitatu inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafungua fursa pana ya ajira hasa kwa Vijana pamoja na kuimarika kwa ufanisi wa kazi katika Taasisi za Umma na hata zile Binafsi.

Akizungumza na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari hapa Nchini mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akitokea Nchini China kwa ziara ya siku Tano ya Kiserikali Balozi Seif  aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, kukamilika kwa eneo la maegesho ya ndege pamoja na Mawasialiano  Serikalini { E. Government }.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kukamilisha taratibu zilizobakia katika hatua za mwisho  kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa eneo la maegesho ya Ndege kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Zanzibar kupitia miradi hiyo itaongeza mapato yake kupitia Sekta ya Utalii, harakati za Kibiashara nah ii itatokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii na wageni watakaoamua kutumia huduma hizo za usafiri wa uhakika.

Akizungumzia Mradi wa Mawasiliano Serikalini { E - Government } Balozi Seif alisema kukamilika kwa mradi huo  awamu ya Pili kwa hatua ya kuunganishwa na mfumo wa Mtandao wa Kisasa utawawezesha Wananchi kupata huduma kwa njia ya mawasiliano.

Alisema Wananchi watapata kuhudumiwa moja kwa moja kwa mfumo wa Internet kwenye sekta za Afya, Elimu pamoja na urahisishaji wa ukusanyaji wa  Mapato ya Serikali Kuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.