Habari za Punde

Serikali ipo mbioni kuandaa sheria ya mfuko wa bima ya afya

Na Salmin Juma, Pemba

SERIKALI YA MAPINDUZI Zanzibar imeandaa rasimu ya sheria ya mfuko wa bima ya afya inayokusudia upatikanaji wa rasilimali fedha endelevu kwa ajili ya uimarishaji wa utoaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wote. .

Mkuu wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla amesema mfuko huo utasaidia kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wanachama wa mfuko huo na kumkinga na matumizi yanayoweza kumuingiza katika umasikini pingi atakapougua yeye na wategemezi wake.

Hayo ameyasema hayo huko ukumbi mdogo wa mikutano wa kiwanda cha mafuta ya makonyo katoka mkutano wa kupitia na kujadili rasimu ya sheria ya mfuko wa bima ya afya kwa maafisa na na wadau wengine wa afya kutoka sekta mbalimbali za umma.

Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa azma hiyo ya Serikali inalenga kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Zanzibar wanafaidika na mfuko huo

Nao baadhi ya wachangiaji wa mapitio hayo wamesema endapo rasimu hiyo itapita nakuwa sheria itatowa mwanga kwa wananchi wa Zanzibar kuweza kumudu huduma za kiafya kwa muda muafaka kwa vile mchangiaji wa mfuko huo huanza kuchangia fedha kabla ya kuugua na hivyo kuondowa hofu ya utafutaji wa fedha za ziada kipindi cha maumivu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.