Habari za Punde

Msiba wa Marehemu Amina Athumani Mwandishi wa Habari za Michezo Gazeti la Uhuru na Mzalendo Kisiwani Zanzibar.

Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.

Kwa taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu utasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana. 

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.
 Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu Ndg Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutowa pole leo asubuhi.
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athuman Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar leo asubuhi kutowa mkono wa pole kwa wafiwa.


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari za Michezo Zanzibar Ndg Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao marehemu Amina Athuman kilichotokea leo asubuhi katika hospitali ya mnazi mmoja.
Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa Kariakoo Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot 
Zanzinews.com.
0777424152 Or 0715424152., 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.