Habari za Punde

Ukosefu wa elimu na pembejeo ni changamoto kwa vikundi vya ushirika

Na Salmin Juma, Pemba

Ukosefu wa elimu na pembejeo za kilimo imekuwa ni changamoto kubwa zinazoikumba vikundi vingi vya ushirika nchini kikiwemo kikundi cha ushirika cha NIA NJEMA kilichopo Shamiani  Chake Chake mkoa wa kusini Pemba kinachojikita zaidi katika ukulima wa mbogamboga ikiwemo tungule na mchicha.

Kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha na uhaba huo wa pembejeo kunaendelea kusababisha mavuno hafifu na nguvu nyingi kupotea hali inayorejesha nyuma jitihada za wanaushirika huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana aliyefika shambani hapo kwa lengo la kuwatembelea kutazama faida na changamoto zinazowakabili wakulima wadogowadogo visiwani Pemba katibu wa ushirika huo Bi.

Slimuu Said Ali amesema, tokea walipoanza kulima hawajawahi kutembelewa na mtu yeyote wala  kupatiwa taaluma juu ya kilimo chao hicho  hivyo wanafanya kazi hiyo kwa mazoea hali inayowapa shida kukabiliana na changamoto za kilimo hasa katika kustawisha vizuri mimea lakini wameamua kufanya tu alimradi wapate chochote wakiamini kinaweza kuwasaidia.

Amesema  kuwa kutokana na ukosefu wa pembejeo ikiwamo vifaa kazi kama vile mipira ya kusambazia maji, dawa  na vyenginevyo  kumepelekea mazao hayo kushambuliwa na wadudu na hatimaye hupata mavuno tofauti na makadirio yao.

Akizungumzia kiwango cha mavuno yao wanayayapata katibu huyo amesema kwa siku huvuna vicha 50 hadi 60 vya mchicha na iwapo kama watapata taaluma na pembejeo  za kutosha basi wanaweza kuvuna zaidi ya hapo.

Bi Fatma Said mwanachama wa wa kawaida katika ushirika hauo amesma lengo la kuanzisha ushirika ni kujikwamua na hali ngumu ya maisha waliyokua wakikabiliana nayo hapo awali .

“kutokana na ugumu wa maisha tuliamua kujikusanya pamoja ili nguvu iwe kubwa na sasa mambo mazuri tunapata alau mahitaji kidgo kama vile kusaidia katika familia”alisema Said.

Aidha Said ametoa wito kwa akina mama,kutokana na ukali wa maisha yalivyo basi ni vyema  kuachana na tabia ya kumtegema mume tu na badala yake waamke na kufanya kazi huku akirudia rudia msemo wake wa kua “mwanamke kaz”.

Kwa upande wake Muzdalifati Ali ambaye naye ni mwanachama wa ushirika huo amesema tokea ajiunge katika ushirika huo hali imekuwa tafauti na zamani sasa anaweza kumudu gharama za mahitaji yake madogo madogo hali iliyokua ni tofauti kabisa na kipindi cha nyuma.

Kwa pamoja wanaushirika hao wa “NIA NJEMA” wametoa wito kwa serikali kupitia sekta ya kilimo na kila mdau katika kilimo kuwatazama kwa jicho la huruma kuwasaidia katika changamoto zao ili wapige hatua zaid za kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.