Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Timu ya Malindi na JKU Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi Imeshinda Bao 1--0.u

Mshambuliaji wa Timu ya Malindi akimpita beki wa Timu ya JKU wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo kwa bao 1--0.
Katika mchezo huo timu zote zimeonesha mchezo safi na wakujiani kwa muda wode wa mchezo huo kwa mashumbulizi kwa kila upande, hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zikiwa sare ya bila kwa bila.
Timu ya Malindi imepata bao lake la kwanza na kuongoza limepatikana katika dakika ya 87 ya mchezo huo kipindi cha pili kupitia mfungaji wake Mohammed Nyasa kwa kupiga krosi hadi golini na kumshinda mlinda mlango wa Timu ya JKU.
Timu ya Malindi kutokana na ushindi huo umepanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya 10 na kujikusanyia pointi 27, katika ligi hiyo.
Mchezaji wa Timu ya JKU akimpita mchezaji wa Timu ya Malindi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu wa Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan Timu ya Malindi imeshinda bao 1-0.












No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.