Habari za Punde

WAZIRI MKUU AONGOZA MATEMBEZI YA KUHAMASISHA UFANYAJI MAZOEZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) wakishiriki katika matembezi ya kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza Mei 04, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, Wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu na kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu. Matembezi hayo ya Kilomita 10 yalianzia Coco Beach hadi Mzunguko wa Hospitali ya Agha Khan na kurudi Coco Beach
Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakishirki matembzi ya kuhamasisha ufanyaji mazoezi ili kujikinga na magonjwa uyasiyoambukiza yaliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es salaam, Mei 4, 2024. Matembezi hayo ya Kilomita 10 yalianzia Coco Beach hadi Mzunguko wa Hospitali ya Agha Khan na kurudi Coco Beach.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (kushoto) wakishiriki mazoezi viungo baada ya Waziri Mkuu kuongoza matembezi ya kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza,  Mei 04, 2024. Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Wanne kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi-SACP Jumanne Muliro. Matembezi hayo ya Kilomita 10 yalianzia Coco Beach jijini Dar es Salaam hadi Mzunguko wa Hospitali ya Agha Khan na kurudi Coco Beach.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuongoza matembezi ya kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza Mei 04, 2024. Matembezi hayo ya Kilomita 10 yalianzia Coco Beach jijini Dar Es Salaam hadi Mzunguko wa Hospitali ya Agha Khan na kurudi Coco Beach. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.