
Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amevitaka vyambo vya habari kuripoti Sera na Ilani ya vyama vya siasa ili Wananchi waweze kupata elimu ya kutosha.
Ameyasema hayo, huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vituo vya Utangazaji Zanzibar.
Amesema elimu hiyo itawawezesha Wananchi kuchaguwa Viongozi wanaofaa.
Aidha amesema baadhi ya Waandishi wanatumiwa na vyama vya siasa katika kueneza propaganda za chuki na uhasama kwa Wananchi.
Amefahamisha kuwa, Tume ya Utangazaji Zanzibar, inadhamana ya kutoa leseni za Utangazaji, kudhibiti shughuli za utangazaji maadili, hivyo amewataka Waandishi kulinda Sera, Usalama, Mila na Utamaduni za Zanzibar.
Hata hivyo ametoa Wito Kwa vyombo vya Utangazaji Zanzibar kuandaa maudhui yanayowahamasisha Wananchi kushiriki katika Uchaguzi kwa Amani na Utulivu.
Aidha amezitaka Taasisi husika na kuandaa mkakati maalum, utakaosaidia kujadili changamoto za kisekta ili kuweza kuenda sambamba na wakati uliopo wa Sayansi na Teknolojia.
Nae Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak, amesema lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha mashirikiano na wadau wa Vituo vya Utangazaji ili kuleta mustakabali mwema kwa tasnia ya habari.
Amesema iwapo Vituo hivyo vitafuata maadili ya Utangazaji ipasavyo, vitasaidia kulinda Amani ya nchi kabla, wakati na baada ya Uchaguzi .
Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Sleiman Ame Khamis amefahamisha kwamba mashirikiano na mshikamano na wadau Mbali mbali utasaidia kuleta maendeleo katika sekta ya Utangazaji.
Nae Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA ) Ofisi ya Zanzibar bi Esuvatie Masinga amesema kuwa wakifanya kazi nyingi ikiwemo kutoa elimu kwa jamii.
Hivyo ameishuru Tume ya Utangazaji Zanzibar na kuahidi kushirikiana ili waweze kutekeleza majuku yao kwa ufanisi
Tunzo mbalimbali zimetolewa ikiwemo, vinara waliotoa huduma bora kwa jamii, vituo vilivyolipa kodi vizuri ambapo Mhe. Tabia ameahidi kutoa fedha ili kuongeza Ari na Motisha katika vituo vya Utangazaji.
Imetayarishwa na kitengo cha habari, WHVUM.
No comments:
Post a Comment