Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa waandishi wa habari kwa kuzingatia sheria na sera na kanuni zilizopo ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab alisema hayo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Alisema hatua hiyo inakuja kwa kufuata sera na kanuni za habari kwa kuweka mazingira bora kwa waandishi ili kutekeleza vyema kazi zao.
Alifahamisha kuwa vyombo vya habari vinamchango mkubwa wa kuchochea maendeleo ya nchi hivyo ni vyema kutumia maadili na uweledi katika utekelezaji wa kazi zao.
Alisema mwaka 1993 Baraza kuu la Umoja wa Mataifa ilianzisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ili kukuza na kuendeleza haki na uhuru wa habari kwasababu dunia ikizingatia nyenzo muhimu ya maendeleo kupitia Nyanja mbalimbali.
Sambamba na hayo alisema tume ya utangazaji inajukumu la
kutoa leseni kwa wawekezaji wenye uwezo wa kuanzisha
vyombo vya habari kwa kuzingatia sera na sheria za vyombo
vya habari.
Akiwasilisha mada ya Historia ya vyombo vya habari
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt.
Abdalla Mohammed Juma alisema Zanzibar inahistori refu
kwa masuala ya mawasiliano kuliko nchi nyengine duniani.
Alisema Zanzibar ni nchi ya mwanzo kusini mwa jangwa la
sahara kuwa na simu inayotumia wayalesi, kiwanda cha
uchapishaji na Televisheni ya rangi, sinema na makapuni na
vyombo vya habari lakini bado kwa sasa kuna changamoto
kwa baadhi ya waandishi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Nae Ofisa Sheria wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Khadija
Mabrouk Hassan alipokuwa akiwasilisha mada ya mabadiliko
ya sera, sheria na kanuni za habari Zanzibar alisema sekta ya
habari ni muhimili mkuu katika kuchochea maendeleo ya nchi
kutokana na kutoa haki ya msingi ya kikatiba.
Alisema sekta ya habari hapa nchini inasimamiwa na sheria ili
kuwawezesha waandishi kutekeleza majukumu yao kwa
uweledi.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari
ni ‘Uwandishi wa Habari na Changamoto ya Mabadiliko ya
Tabia Nchi’.
No comments:
Post a Comment