Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Akitangaza Kifo cha Mzee David Msuya Ikulu Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya kilichotokea leo tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo. Taarifa zaidi ya Mipango kamili ya msiba itaendelea kutolewa na Serikali.

Rais Dkt. Samia ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 7 hadi 13 Mei, 2025.

Rais Dkt. Samia anawapa pole Ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.