Habari za Punde

Dk. Shein Atembelea Maeneo Yalioathirika na Upepo Nyarugusu Wilaya ya Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe leo alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  wananchi ambao Nyumba zao zimepata athari ya kun'goka kwa mapaa   kutokana na Upepo mkali uliosabisha   na  uharibifu   huo jana, ambao  umepelekea kukosa pahala pa kuishi,[Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Wataoto wa maeneo ya Nyarugusu Wilaya ya Mjini,Unguja wakimuangalia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe kuwafariji na kutoa pole kwa wananchi walioathirika na Nyumba zao zilizobomoka kutokana na Upepo mkali uliotokea jana katika maeneo yao na kupelekea uharibifu kwa kung'oka mapaa ya Nyumba wanazoishi, wakati alipofanya ziara maalum leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Vijana waliojitolea kutoa msaada kwa Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kung'oka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana, alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  wananchi hao leo alipofika kutoa mkono wa pole
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na  kuwasalimia Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kung'oka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana, alipofika   kuwafariji na kuwapa pole kutokana mtihani walioupata,alipokuwa katika ziara maalum  leo akiwa na Viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo
Miongoni mwa Nyumba zilizoharibika kutokana na Upepo Mkali ulitokea jana katika maeneo ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea Wananchi kukosa maakaazi ya kuishi,hali hilo aliiyona Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati alipofanya ziara maalum leo katika Shehia hiyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Nd,Abdalla Ali Mohamed Mwananchi wa Makondeko Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakati alipofika Nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa Wananchi waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,Rais alifika katika shehia hiyo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  Wananchi, na  kutoa mkono wa pole,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud

1 comment:

  1. Hongera Mh Rais, ila nina suali hivi majina ya mitaa zanzibar yamekwisha Nyarugusu Makondeko ndio nn. Tuache kuiga

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.