Habari za Punde

Waziri wa Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Akiwasilisha Mswada wa Sheria.

Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman akiwasilisha Mswada wa Sheria ya (Marekebisho) ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nam.4 ya Mwaka 2015, wakati wa Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar unaofanyika katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.  
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiongoza Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi katika Ukumbi wa Baraza akifuatilia hutuba ya Mswada wa Sheria ukiwasilishwa na Waziri husika kwa Wajumbe wa Baraza. 
Waziri Haroun Ali Suleiman akisoma mswada huo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kuuchangia na kuupitisha wakati wa mkutano huo wa Sita wa Kupitisha Bajeti za Wizara za Serikali ya SMZ, Unaoendelea na kuwasilisha Bajeti ya Wizara mbalimbali kwa Wajumbe na kuzichangia 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia mkutano wa Sita wa Baraza wakati ukisomwa Mswada wa Sheria ya Viongozi wa Umma kwa Wajumbe.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibare Mhe. Simai Mohammed Said akifuatilia Mswada huo kwa makini ili kuweza kuuchangia wakati ukifika.
Wajumbe wakifuatilia mswada huo wakati ukiwasilishwa katika mkutano wa Baraza. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitoka katika ukumbi wa Mkutanio wa Baraza baada ya kuahirisha kwa mapumziko ya mchana baada ya kuwasilishwa Mswada wa Sheria ya Viongozi wa Umma katika mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitoka katika Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana na kuendelea na mkutano huo jioni kwa kuchangia Mswada wa Sheria ya Viongozi wa Umma.
Waziri Haroun Ali Suleiman akitowa katika ukumbi wa mkutano wa baraza akiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe Dk Mwinyihaji Makame Mwadini.
Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar  Mhe Abdallah Maulid Diwani akiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf, baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa Baraza la Wawakilishi kwa mapumziko ya mchana.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said akimsikiliza Waziri Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe. Salama About Talib wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Balozi Amani Salum Ali akisisitiza jambo wakati akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidh wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa baraza baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe Salama Aboud Talib nje ya ukumbi wa mkutano wa baraza baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.