Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Atowa Mkono wa Eid Fitri kwa Wazee na Watoto Yatima Zanzibar.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimpa mkono wa Eid El Fitri mmoja wa Wazee wanaoishi katika Kijiji chiji cha Wazee Welezo Zanzibar Bi. Saada  alipofika kuwatembelea na kuwajulia hali na kutowa mkono wa Eid Fitri kwa wazee hao wanaoishi katika kijiji hicho cha welezo Zanzibar. wanaoishi wazee wasiojiweza 
MKE  wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimpa mkono wa Eid Fitri Mzee wa Kijiji cha Wazee Welezo Rashid Salum (Kassika) alipofika kutowa mkono wa Eid kwa Wazee hao
MZEE wa Nyumba za Wazee Sebleni Bi. Asaa Ali Issa akitowa neon la shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika kuwatembelea na kuwapa mkono wa Eid Fitri katika makaazi yao sebleni Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitowa mkono wa Eid Fitri kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa alipofika kuwatembelea na kutowa mkono wa Eid Fitri kwa watoto hao
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa amemchukuwa Mtoto aliyetupwa katika kijiji cha Bungi Wilaya ya Kati Unguja  amepewa jina la Wahida Abdalla akiwa na miezi (4) kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na kulia Waziri wa  Kazi Vijana na Uwezeshaji Wazee na Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico. 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitowa mkono wa Eid El Fitri kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.