Habari za Punde

Fomu za kugombea uchaguzi Jumuiya ya wazazi zaanza kutolewa kisiwani Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

JUMUIYA ya Wazazi ya CCM wilaya ya chakechake  mkoa wa kusini Pemba imewataka wanachama wa  jumuiya hiyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi tofauti za uwongozi ili kukijenga chama hicho hatimae kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa jana na katibu wa wazazi wilaya ya chakechake Bikiembe Ramadhan Khamis katika zoezi la ugawaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika jumuia hiyo, zoezi ambalo limeanza rasm tarehe 2 jully 2017.

Akimkabidhi fomu ya ugombea nafasi ya wajumbe wawili wa halmashauri kuu wilaya ya chakechake mmoja miongoni mwa wagombea hao Bimkubwa Rajab , Bikiembe  amefahamisha kuwambia wagombea hao kuwa, katika kinyang'anyiro hicho kuna kupata na kukosa, hivyo kwa wale wote watakaokosa nafasi wanazozigombania wasiwe wenye kuvunjika moyo na badala yake waendelee na utumishi mzuri katika chama kwani haiwezekani kupata wote waliyojitokeza kuomba.

Akipokea fomu hiyo Bimkubwa Rajab ametoa wito kwa wanachama wenzake kumunga mkono ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo huku akiahidi kuingia vijijini kuwatafuta akina mama kuwashajihisha kujiunga na chama sambamba na kuwasemea changamoto zao zinazowakabili.

Kwa pande wake Seif Kassim mwanachama wa chama hicho anaegombea uwenyekiti wa wazazi wilaya ya chakechake  amesema, ni vyema kwa wanachama hicho kuutumiwa wakati huu kugombea nafasi mbalimbali za uwongozi kwani kutaleta maendeleo makubwa katika chama.

Amesema ikiwa kuna mwanachama kiupande wake anaona kuna  kiongozi hatekeleza majukumu  ipasavyo basi huu ndio wakati muwafaka  kuchukua fomu na kugombea ili kurekebisha pale ambapo aliona hapakua sawa.

Kila baada ya  miaka mitano chama cha mapinduzi CCM na jumuiya zake  hufanya chaguzi za viongozi mbalimbali ikiwa ni katika muendelezo wa matumizi ya democrasia katika chama hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.