Habari za Punde

Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town Development Kufanya Maonesho ya Mradi huo Kwa Wananchi wa Zanzibar

Chief Operating Officer, Tobias Dietzold akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandali ya kufanya maonesho ya Siku mbili kutoa fursa kwa Wananchi wa Zanzibar kutembelea eneo hilo la Mradi huo wa nyumba za kisasa kwa ajili ya biashara kwa Wananchi wa Zanzibar na wa Nje ya Nchi, Amesema wananchi watapa fursa ya kuuliza maswali na jinsi kupata nyumba hizo kwa ajili ya makazi. mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Mradi huo migombani Zanziba.
Mr. Tobias Dietzold akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusiana na Mradi huo wa Fumba Town Development kuhusiana na kukamilika kwa maonesho hayo na kutowa usafiri bure wa kwenda na kurudi fumba na kuandaliwa vituo maalumu siku hiyo vya kupandia magari. 
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo kwa makini ili kutowa taarifa ilio sahihi kwa wananchi kuhusiana na Mradi huo wa Nyumba za Kisasa katika maeneo fumba Nje kigodo ya Mji wa Zanzibar.
 Meneja Mauzo ( Sales Manager), Said Ally Said akitoa ufafanuzi wa Maelezo ya Mradi huo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo katika eneo la Migombani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.