Habari za Punde

Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuiya na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu Yakutana Jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella, akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha  wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo () na Mkurugenzi Mradi wa kuzuia biashara hiyo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI,Dk. Lyungai Mbilinyi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mradi wa Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI,Dk. Lyungai Mbilinyi,akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha  wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, na Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,akizungumza wakati wa mkutano wa  kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mmoja kati ya wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,Bi Nasima Chum akizungumza wakati wa Kikao cha kupitia Sheria inayosimamia biashara hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,wakiwa katika majadiliano wakati wa Kikao cha kupitia Sheria inayosimamia biashara hiyo. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
 Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.