Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Simba Yabanwa na Mlandege Katika Mchezo wa Kirafiki Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba jana imebanwa mbavu na watoto wa Abdul Satar timu ya Mlandege baada ya kutoka sare tasa 0-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Amaan saa 2 za usiku.
Simba iliwachezesha nyota wake kadhaa wapya akiwemo Mlinda Mlango Aishi Manula, mlinzi Salim Mbonde pamoja na kiungo Haruna Niyonzima huku washambuliaji wake wapya hatari Emmanuel Okwi pamoja na John Bocco hawakucheza.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba kucheza Visiwani hapa ndani ya msimu huu mpya ambapo pia ni mchezo wake wa tano wa kirafiki katika kipindi hichi cha kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2017-2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.