










MAKAMU wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu leo amezinduwa rasmi Tamasha la
Jinsia Tanzania mwaka 2017. Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya TGNP
Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na uzinduzi huo ameongoza zoezi la
kutoa tuzo kwa baadhi ya akinamama waliofanya vizuri na kutoa mchango katika
maendeleo ya wanawake.
Akizungumza kabla ya uzinduziwa tamasha hilo, Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu
aliipongeza TGNP kwa harakati zake za kuiunga mkono na kuikosoa serikali pale
wanapoona imekwenda tofauti.
Alisema kitendo cha kukemea na kutoa
mapendekezo na suluhisho sehemu ambayo wanaamini serikali haijafanya vizuri ni
kitendo cha kiungwana na kinachochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Alisema hatua tuliofikia sasa si ya kulaumiana bali kushirikiana katika kuliletea taifa
maendeleo. Alisema Serikali ya Jamhuri ya Tanzania inatambua umuhimu wa
kuzingatia usawa wa jinsia katika kuchangia na kuendeleza maendeleo ya taifa kwa
ujumla.
Alisema Serikali tangua uhuru hatua kwa hatua imekuwa ikizingatia
utungwaji wa sheria na kanuni rafiki zinazosimamia usawa wa jinsia.
Aliongeza Tanzania kama mwanachama wa UN na AU imekuwa imeridhia mikataba
na itifaki na makubaliano mbalimbali ya kimataifa na kikanda kuhusiana na usawa
wa jinsia na uwezeshaji wanawake, utekelezaji wa makubaliano ya uringo wa
Beingin, Malengo ya Maendeleo Endelevu pamoja na mkataba wa kupinga aina zote
za ubaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule aliwataja na
kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali ambapo Makamu wa
Rais alikabidhi tuzo kwa wakinamama hao. Miongoni waliopokea tuzo ni pamoja na
Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Suluhu, aliyekabidhiwa tuzo yake na Mwenyekiti
wa bodi.
Wengine ni pamoja na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda, Mbunge
wa Bunda Mjini, Estar Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester Mwaikambo, na
Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada walizozionesha katika uongozi na
wote walipewa tuzo.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akicheza na wasanii na wageni waalikwa.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia)
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zipora Shekilango (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marry Lusimbi (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.width="500"]
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu kwa kufanikiwa kuwawezesha akinamama.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri Kisarawe.[/caption]
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi daktari wa kwanza mwanamke Tanzania, Dk. Ester Mwaikambo (kulia)
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi mbalimbali na shughuli za akinamama wanaharakati ngazi ya jamii za kujikwamua.










No comments:
Post a Comment