Habari za Punde

Meli ya Kifahari Kutoka Nchini Oman Yawasili Leo Zanzibar Kwa Ziara ya Siku Sita

-Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH ikiingia katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman ikiwa na Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo,ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi  Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman.

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi wapili kushoto akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumh mara baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi kulia akizungumza kitu akiwa pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi mara baada ya kuteremka katika Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi akiwa pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakitembelea vikundi mbalimbali vya Ngoma ya Utamaduni mara baada ya kuwasili kwa Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi kulia akisalimiana na Mabaharia mara baada ya kuingia katika Meli ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliofika katika Bandari ya Zanzibar pamoja na Waziri wa Mafuta na Gesi  wa  Serikali ya Oman kwa Ziara ya Siku Nne ikiwa na lengo la  kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi katikati akiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumh wa mbele mara baada ya kuingia katika Meli  ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliofika zanzibar wakiwa na ziara ya siku Nne kwa Lengo la kuimarisha umoja Amani na Upendo Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.