TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, leo
amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za serikali kama
ifuatavyo:-
1. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu
cha 7(1) cha Sheria ya Baraza la Michezo Namba 5 ya 2010, Rais Mheshimiwa Dkt.
Shein amemteua Bwana Gulam Abdulla Rashid kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo,
Zanzibar.
2. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu
cha 7(2) cha Sheria ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Namba 3 ya mwaka 2009, Rais
Dkt. Shein amemteua Meja Jenerali Mstaafu Said S. Omar kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini.
3. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu
cha 5 (2) cha Sheria ya KMKM Namba 1 ya 2003, Mheshmiwa Rais Dkt. Shein
amemteua Kapteni Khamis Simba Khamis kuwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Kuzuia Magendo (KMKM).
4. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu
cha 12 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Namba 3 ya 2015, Rais Dkt.
Shein amemteua Ndugu Farhat Ali Mbarouk kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira
katika Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.
5. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu
cha 5(1) cha Sheria ya Shirika la Nyumba Namba 6 ya 2014, Mheshmiwa Rais
amemteua Ndugu Riziki Jecha Salim kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba
katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu
15(1) cha Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 8 ya 2014, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Ndugu Mkufu Faki Ali
kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Wete, Pemba.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Abdulhamid
Yahya Mzee, uteuzi huo unaanzia leo tarehe 17 Oktoba, 2017.
No comments:
Post a Comment