Habari za Punde

Tangazo kwa Umma Kuhusiana na Ujazaji wa Fomu Kwa Njia ya Kielektroniki.Kuomba Passport.

IDARA YA UHAMIAJI
TANGAZO KWA UMMA:
IDARA YA UHAMIAJI ZANZIBAR, INAWATAARIFU KWAMBA IMEANZISHA HUDUMA YA KUJAZA MAOMBI YA PASIPOTI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI KUPITIA TOVUTI YAKE; www.immigration.go.tz. HII NI HUDUMA MPYA INAYOMUWEZESHA MUOMBAJI KUJAZA FOMU HIYO POPOTE ALIPO.
MUOMBAJI BAADA YA KUJAZA FOMU HIYO NA KUAMBATISHA PICHA YAKE KAMA ATAKAVYOELEKEZWA MTANDAONI, ATATAKIWA KUICHAPISHA “PRINT” FOMU HIYO NA KUIWASILISHA KATIKA OFISI YA UHAMIAJI ILIYOPO KARIBU NAYE PAMOJA NA VIELELEZO HUSIKA, KWA MUJIBU WA MADHUMUNI YA SAFARI YAKE.  

MADHUMUNI YA HUDUMA HII, KUONDOA USUMBUFU KWA MTEJA KWENDA OFISI ZA UHAMIAJI KUCHUKUA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI NA PIA ITAMUWEZESHA MTEJA KUFUATILIA HATUA LILIPOFIKIA OMBI LAKE, KWA NJIA YA MTANDAO. AIDHA HUDUMA HII HUSAIDIA KATIKA KUIMARISHA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MWOMBAJI KIELEKTRONIKI.
HIVYO, KUANZIA TAREHE YA TANGAZO HILI IDARA, INAWATAKA WAOMBAJI WOTE WA HUDUMA YA PASIPOTI ZANZIBAR, KUJAZA FOMU ZA MAOMBI KWA NJIA HIYO YA KIELEKTRONIKI.
IMETOLEWA NA;
 KITENGO CHA UHUSIANO,
AFISI KUU YA UHAMIAJI, ZANZIBAR.

18 OKTOBA, 2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.