Habari za Punde

Mkutano wa Mafunzo ya Hati Miliki Kwa Wadau Wafanyika Zanzibar leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutamo wa mafunzo ya kuelewa Hati Miliki kwa Wadau mbalimbali Zanzibar kuhusiana na Kopi Riiti za wamiliki wa Muziki na Vitabu Zanzibar, Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Hati Miliki Zanzibar ( COSOZA) kwa pampoja na World Intellectual Property Organization (WIPO) mafunzo hayo ya Siku mbili yanafanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru Hurumzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hati Miliki Zanzibar (COSOZA) Iddi Suweid akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa mafunzo ya kufahamu hati miliki kwa Wadau mbalimbali wanaotowa huduma ya kijamii kupitia kazi za Wasanii Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hati Miliki Zanzibar COSOZA Mtumwa Khatib Ameir akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa maelezo ya Hati Miliki kwa watumiaji wa kazi mbalimbali zinazotolewa na Wasanii. 
MWAKILISHI kutoka WIPO Geneva Sinior Program Offece. Sonia Cruickank, akizungumzia Hati Miliki matumizi ya Hati Miliki kwa Wadau waliohudhuria Mafunzo hayo kutoa Elimu jinsi ya uhalali wa mmiliki wa kazi na kutumimwa na mtu mwengine bila ya ridhaa yake na inaposwa kumlipa mmiliki halali, mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Marumaru Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mafunzo hayo ya Siku Mbili kwa Wadau na Wasanii mbalimbali wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa Siku Mbili yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Marumaru Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.