Habari za Punde

Makamu wa Rais, mama Samia aendelea na ziara kisiwani Pemba

 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikagua ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni, akiwa amefuatana na viongozi mbali mbali wakiwemo Naibu waziri wa elimu na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maeleo ya ujenzi wa skuli mpya ya Sekondari ya Micheweni, kutoka kwa mmoja ya maijinia wa Wizara ya Elimu, ikiwa mwendelezo wa ziara yake ya Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MUONEKANO wa baadhi ya madarasa yanayoendelea kujengwa katika skuli ya Sekondari Micheweni, kama yanavyoonekana katika picha wakati wa ziara ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Naibu waziri wa Afya Harous Said Suleiman, wakati alipowasili katika uwanja wa Shamemata kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Micheweni katika ziara yake ya Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari na Msingi Micheweni, wakisikiliza kwa makini hutuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed katikati na kushoto ni Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Injinia Hamad Yussuf masauni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 NAIBU waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri, akutoa maelezo ya Wizara ya elimu juu ya mikakati yake katika utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili katika uwanja wa Shamemata Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed, akizungumza na wananchi wa Micheweni katika uwanja wa Shamemata, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Micheweni katika mkutano wa dhara uliofanyika kiwanja wa Cha Shamemata.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Mikoba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, wakati apomalizia kuzungumza na wananchi wa Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Makawa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, wakati apomalizia kuzungumza na wananchi wa Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.