Habari za Punde

Kampuni ya PennyRoyal Limited Zanzibar Kupitia Mradi Wake wa Best Of Zanzibar. Yatowa Msaada wa Ujenzi wa Kituo cha Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa wa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar Aminata Kaeti,alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar,kuweka jiwe la msingi.jengo hilo limejengwa na kampuni hiyo kupitia Mradi wake wa Kusaidia Jamii katika Afya Jamii, Elimu na Mazingirana Ajira unaojulikana kwa Best of Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Kichama Abdi Ali Mzee (Mrope) wakati akiwasili katika viwanja vya ujenzi wa Kituo cha Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar kuweka jiwe la msingi la jengo hilo lililojengwa kwa Msaada na kupitia Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, kwa ajili ya Watu Wenye Ulemavu kuwawezesha kutumia jengo hilo kwa miradi yao mbalimbali kujikimu kimaisha.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kipazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar, akiwa na Afisa wa Kampuni ya PennyRoyal Zanzibar Aminata, na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati wa ziara yake Kisiwani Unguja. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea jengo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi akipata Maelezo kutoka kwa Katibu wa Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Said Yakuob. 
Viongozi wa CCM wakiwa katika ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakitembelea jengo hilo baada ya uwekaji wake wa jiwe la msingi.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Unguja. Mzee Kai Makame Kai, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo hilo katika mtaa wa shauri moyo. 
Afisa wa Kampuni ya PennyRoyal Limited Zanzibar Aminata akitowa maelezo ya Mradi wa ujenzi wa Jengo la Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo linalojengwa kupitia Mradi wa kusaidia Jamii wa Afya Jamii, Elimu, Mazingira na Ajira wa Best of Zanzibar,  
Mwenyekiti wa Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar Mzee Kai Makame Kai, akitowa shukrani kwa  Wajenzi wa jengo lao hilo linalojengwa na Kampuni ya PennyRoyal kupitia Mradi wake wa Best of Zanzibar, na kutowa shkrani kwa niaba ya wanachama wake, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu.Zanzibar. 
Mtaalamu wa lugha za alama kwa viziwi akitowa ishara wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kituo cha Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la ShauriMoyo Zanzibar, wakati Mgeni rasmin akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la mzingi la Jengo la Watu Wenye Ulemavu wa Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar, wakati wa ziara yake Kisiwani Unguja.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.