Habari za Punde

Aokotwa akiwa ameshafariki dunia

na Salmin Juma , Pemba
Mtu mmoja mkaazi wa nyumba za wazee wete aliyejuulikana kwa jina la Masri Hamad Ali Rubeya (72) ameokotwa katika jumba bovu (gofu) akiwa ameshafariki dunia huku kichwani mwake akionekana kuwa na majeraha na damu zikimchuruzika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba Shehan Mohd Shehan amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema, limetokea majira ya saa 5 za asubuhi jana maeneo ya chachani chakechake katika jengo lililo mkabala na jengo la CCM.
Baadhi ya mashuhuda wakiwamo maafisa wa jeshi la Polisi na waandishi wa habari wakiitazama maiti iliyopo chini
Kamanda shehan alisema, watoto waliyokua wakipita katika jengo hilo ndio waliyomuona mtu huyo na kupiga kelele ambapo kulikua na askari wa jeshi la polisi , alisikia kelele hizo na ndipo alipoamua kwenda na kushuhudia na kutoa taarifa kituoni.
Akiendelea kueleza kamanda alisema baada ya uchunguzi kufanyika walibaini kuwa Masri aliuliwa sehemu nyengine na hapo alikwenda kutupwa na jeshi la polisi litawasaka wote waliyohusika na tukio hilo.
“kichwani na usoni amechomwa na kitu chenye ncha kali na inaonekana hapo kenda kutupwa tu “alisema kamanda.
Katika hatua nyengine kamanda shehan alisema mpaka sasa maiti hospitali ya chakechake na jamaa zake bado hawajajitokeza .
Muoneokano wa ndani wa jumba (gofu) ambalo mtu huyo aliyeokotwa maiti alimo patikana
“ikiwa kama jamaa zake hawajajitokeza basi kutafanyika taratibu ili achukuliwe na ustawi wa jamii mana alikua akiishi katika nyumba za wazee wete “ alisema kamanda.
M/kiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya chakechake Mh : Rashid Hadid Rashid alikua ni mmoja katika ya waliyoishuhudia maiti ya mtu huyo na alipolulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya matukio hayo kushuhudiwa nchini alisema, hayo si matukio yaliyozoeleka kutokea nchina na ni matukio ya kuhuzunisha.
“jeshi la polisi lihakikishie wanalifanyia kazi tukio hilo ili wahusika wpatikane na isheria ichukue mkondo wake” alime Mh Hadid

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.