Habari za Punde

Vifaa Vya Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bububu Hadi Mkokotoni Vya Kampuni ya Kichina Inayojenga Barabara Hiyo ya China Civil Engineering Construction Corporation. Vyawasili Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akimsikiliza Afisa wa China Civil Engineering Construction Corporation, Logistic Manager East Africa Limited Mr. David Yan, akitowa maelezo ya dokumenti ya Vifaa vya Kampuni yake vilivyowasili Zanzibar kwa Meli ya Mizigo ya Cosco Shipping ikitokea Nchini China.kwa ajili ya Utengenezaji wa Mradi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Baada ya kushinda Tenda ya utengenezaji wa barabara hiyo inayojumuisha barabara tatu.
Magari ya Kampun i ya China Civil yakiteremshwa katika bandari ya Zanzibar yakitokea Nchini China kwa ajili ya kutumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kuazia Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakitembelea Meli ya Cosco Shipping kutoka Nchini China ilioleta Vifaa vya utengenezaji wa Mradi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati ilipowasili katika bandari ya malindi Zanzibar kushusha vifaa hivyo.
Mitambo ya kupikia lami ikiwa katika Meli ya Cosco Shipping ikiwa katika Bandari ya Malindi Zanzibar kwa ajili ya kuvishusha kuaza kazi ya utengenezaji wa barabara hiyo.


Magari ya Kampuni ya China Civil yakiwa katika kambi ya Kampuni hiyo katika eneo la Kandwi kwa ajili ya kuaza kazi hiyo ya Ujenzi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akiwa na Afisa wa Kampuni ya China Civil Mr. David Yan, akitembelea kambi hiyo kuona maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni na kuridhika na maandalizi hayo yakiwa yamekamilika kwa kiasi kikubwa na kuaza kwa Mradi huo unaotegemea kuaza mwezi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni inayojengwa na Kampuni ya Kichina ya China Civil Enineering Construction Corporation, kulia ni Afisa wa Kampuni ya China Civil Mr. David Yan na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Shomari, wakifuatilia mkutano huo na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Kisauni Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Bububu hadi Mkokotoni inayojengwa na Kampuni ya Kichina ya China Civil Enineering Construction Corporation, wakifuatilia mkutano huo na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Kisauni Zanzibar.
 Afisa wa Kampuni ya China Civil Mr. David Yan na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Shomari, wakifuatilia mkutano huo na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Kisauni Zanzibar.

1 comment:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.