Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakunga na Wauguzi Zanzibar.Bi. Valeria Rashid Haroub akikabidhi Msaada wa Vyakula kwa Afisa wa Ustawi wa Jamii Zanzibar Kitengo cha Watoto Yatima Mazizini Ndg. Juma Makame Kombo,wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Vyakula na kutoka huduma za kuwapima Afya zao walipowatembelea na kukabidhi msaada huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakunga na Wauguzi Zanzibar.Bi. Valeria Rashid Haroub akiwa katika picha ya pamoja na Watoto Wanaoishi katika Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa Vyakula na kuwapima Afya Zao.(Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).
BARAZA la Wakunga na Wauguzi imefanya ziara ya kuwatembelea watoto yati ma wanaolelewa katika kituo cha Watoto Mazizini Zanzibar kujua maendeleo yao kiafy a pamoja na kutowa huduma mbalimbal i za kuchunguza Afya zao.
Aidha, katika ziara hiyo, wauguzi waliwapima afya, uzito ili kufahamu kama wanakabili wa na maradhi mbalimbali, pamoja na kutoa tiba.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa baraza hilo Bi.Valeria Rashid Haroub, alisema ziara hiyo ni miongoni mwa s hughuli mbali mbali zinazofanyika kuelekea siku ya wakunga duniani, ambayo itafikia kilele chake Mei 5, 2018.
Amesema watoto ni viumbe wanaohita ji huduma na uangalizi wa mara kwa ma ra ili kutambua afya zao, akieleza kuwa, hatua ya kuwapima maradhi ikiwemo k isukari na kujua viwango vyao vya da mu, inarahisisha kuwaanzishia tiba map ema kabla hali zao hazijawa mbaya.
“Mtoto ni tegemeo la jamii kwa siku za baadae. Anahitaji huduma zote muhimu ikiwe mo malazi,elimu, afya na ishe bora kama alivyomalengoyaserikali,” alisemaMwenyekitihuyo.
Nae Msaidizi mrajisBaraza la wauguzi Rajab KhamisRajab alisema watoto ni muhimu hivyo wana hitaji kupewa huduma zote za jamii.
Akizungumziamaadhimishoyasikuy aWakunganaWauguzi, Valeria alisema baraza hilo limepanga kufa nya shughuli mbalimbali ikiwemo ku tembelea maskulini kwa ajili ya kut oa elimu kwa wanafunzi juu ya kujiki nga na maradhi tafauti hasa ya mripu ko katika kipindi hichi cha mvua.
Aidha, alisema wamejipanga kutoa elimu ya uzazi wa mpango katika vituo mbalim bali mijini na vijijini na kuwashaj iisha akinamama kujifungulia hosp itali ilikupunguza matatizo yanay oweza kujitokeza wakati wa kujifun gua.
“ Serikaliimewekavituovyaafyavin avyotoahudumaza mama namtotokilasehemuilikuwarahisi shiauzazisalama,” alisema Valeria.
Alizitaja miongoni mwa hospitali z itakazotolewa huduma hizo pamoja n a elimu kuwa ni Makunduchi Mkoa wa K usini na Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Hatahivyo, aliwatalawakunganawauguziwasik aevituonikusubiriwananchiwanao fuatahuduma, bali wapite nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya afya, uzazi wa mpango pamoja na maradhi me ngine.
Katikaziarahiyo, wakunganawauguzihaowalitoazawa dikadhaazakwawatoto, ikiwemobiskuti, maziwa, madaftarinanyenginezo.
“ Kauli mbiu ya mwaka huu ni wakunga hu ongeza njia katika utoaji wa huduma bora.”
No comments:
Post a Comment