Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Afanya Ziara Kisiwani Pemba na Kukabidhi Msaada

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiangalia moja ya Sabuni za kuogea watoto, zilizotolewa na Mfanya Biashara Maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (Bopar) kwa Hospitali ya Wete
OFISA Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Shadiya Shaban Seif, akimkabidhi dawa za watoto Daktari dhamana wa Hospitali ya Wete Khamis Rashid Salum, zilizotolewa na Mfanya biashara maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (bopar), huku Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akishuhudia makabidhiano hayo
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Ofisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Shadiya Shaban Seif, mashine ya kusukumia maji iliyotolewa na Mfanya biashara maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (Bopar) kwa ajili ya Hospitali ya Wete
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Shadiya Shaban Seif, moja ya magodoro yaliyotolewa na Mfanya biashara maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (Bopar) ambapo alitoa magodoro 100, mashuka 100, mito 95, dawa, sabuni na mashine ya maji kwa Hospitali ya Wete 
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, akimkabidhi zawadi mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wete, msaada huo uliotolewa na Mfanya biashara Maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (bopar) kwa wagonjwa wa Hoapistali ya Wete
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, akimkabidhi zawadi mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wete, msaada huo uliotolewa na Mfanya biashara Maarufu Zanzibar Said Nassir Nassor (bopar) kwa wagonjwa wa Hoapistali ya Wete.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimjulia hali bibi Mwazume Bakari aliyelazwa katika Wodi ya Wanawake ndani ya Hospitali ya Wete.
Picha na Abdi Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.