Habari za Punde

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Tawi la Zanzibar Yawatoa Wasiwasi Wananchi Kuhusiana na Utapeli wa Njia ya Mtandao.

Na Takdir Ali. Maelezo Zanzibar. 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Afisi ya Zanzibar imewatoa hofu Wananchi wanaofanyiwa Utapeli kwa njia ya Mtandao na kusema wameandaa utaratibu wa kuwafikisha katika vyombo vya Sheria watakawabaini.
Amesema kumejitokeza makundi ya matapeli wamekuwa wakiwaibiwa watu kwa njia ya Mtandao hivyo serikali haitokubali kuona Wananchi wake wanafanyiwa vitendo hivyo.
Akizungumza na Wanawake Wajasiriamali katika Wilaya ya Kati Meneja wa Mamlaka hiyo afisi ya Zanzibar Esuvitie Msuya huko Dunga Wilaya ya Kati amewataka Wananchi watakaofanyiwa vitendo vya utapeli wapeleke malalamiko yao Kituo cha Polisi sio kulalamika mitaani.
Mkurugenzi huyo amewahakikishia kuwa kitendo cha Wananchi kutumia Mitandao haikubaliki hata kidogo kwani inasababisha kuongezeka Umasikini katika jamii hasa Wakaazi wa Vijijini.
Amesema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwa madai ya kufanyiwa utapeli kupitia mitandao ya simu kwa kupigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi na tayari wameamua kuyafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu na Sheria za nchi.
Amesema kitu cha kwanza Wanachohitaji kufanya mara wanapoibiwa ni kuenda katika kituo cha Polisi kwa hiyo TCRA imekuwa haifanyi kazi pekee bali inashirikiana na Jeshi la Polisi ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Amewashauri Wanawake kufahamu kuwa simu ni mali ya kwao hivyo wasiwaazime watu kwani simu ni kama Silaha ukiitumia vibaya inaweza kuleta athari sambamba na kusajili laini zao na waunge mkono Udhibiti wa Simu kwa Majina yao matatu.
Akielezea wanaotumia Mitandao ya kijamii kama vile Wasap wasiweke Taafifa zao kamili na wawe makini sana kwani Dunia imekuwa kama kijiji.
Nao Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wa Wilaya ya Kati wamesikitishwa na kitendo cha kupigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi wakitakiwa kutuma pesa kwa madai ya ku wengine wamepata ajali au wafanye biashara jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma na kuwakatisha tamaa.
Aidha wamesema wamekuwa wakichukuwa mikopo na kuanzisha Biashara ndogo ndogo lakini kitendo cha kuibiwa kimekuwa wavunja moyo hasa ukichukuwa wengine wamekuwa wakitumia Imani za kishirikina na kuiomba Serikali iwasaidie.
        Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.